24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Nzuki: Waandishi wa habari tumieni kalamu kutangaza utalii

Na Mwandishi Wetu, Ngorongoro

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk Aloyce Nzuki amewataka waandishi wa habari kutumia kalamu zao kujenga taswira chanya ambayo itasambaa duniani kwa ajili ya kutangaza sekta ya utalii.

Dk. Nzuki ametoa kauli hiyo wilayani Ngorongoro wakati wa kufungua kikao kazi cha wahariri na waandishi wa habari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari leo Desemba 28, 2020.

Amesema taswira nzuri itasaidia kutangaza vivutio vingi vya watalii vilivyopo nchini na kusaidia kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali.

Amesema hivi sasa asilimia 80 ya watalii wanaokuja nchini ni wapya na wa zamani ni asilimia 20, jambo ambalo waandishi wa habari wanapaswa kufanya kazi kubwa ya kuendelea kutangaza vivutio vilivyopo.

Alisema waandishi wahakikishe asilimia ya watalii wa zamani inapanda kwa sababu itasaidia kupata watalii wengi zaidi.

Amesema asilimia 70 ya watalii duniani wanapata taarifa kwa kusikia mtu anasema Tanzania kuna vivutio.

Amesema moja ya malengo hayo, ni wizara kutelekeza ilani ya CCM ya mwaka 2025 ambayo inataka wizara kufikisha idadi ya watalii milioni 5 na kufikisha mapato ya Dola za Marekani bilioni 6.

Amesema malengo hayatafikiwa endapo kila upande yaani waandishi wa habari, mamlaka na wadau kila mmoja akijivutia upande wake.

Kwa upande wake, Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Ngorongoro (NCAA), Dk. Fredy Manongi amesema kumekuwapo na ongezeko kubwa la idadi ya watu kwani wakati mamlaka inaanzishwa mwaka 1959 walikuwapo 8,000 sasa wamefika 100,000.

Amesema idadi hiyo inaathiri shughuli za uhifadhi na hatima ya Ngorongoro kwa vizazi vijavyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles