23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

CEGODETA YAVISHAURI VYAMA  UFUMBUZI WA MATATIZO

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam



TAASISI ya Utawala Bora na Maendeleo Tanzania (CEGODETA) imetoa angalizo kwa vyama vya siasa nchini kuwa makini katika masuala ya kuvuana uanachama au kufukazana.


Imesema mambo hayo yana hatari kubwa ya kudhoofisha vyama husika na kujenga maadui zaidi ndani ya vyama hivyo.
Mkurugenzi wa CEGODETA, Thomas Ngawaiya, alikuwa akizungumzia masuala mbalimbali yanayohusiana na uendeshaji wa vyama vya siasa nchini.


Alisema badala ya  kufikia uamuzi kama huo ambao ni mzito ni vizuri kutafuta namna ya kuleta muungamo ndani ya vyama husika, kuwashinda maadui.


Ngawaiya ambaye ni mwanasiasa mkongwe alitoa mfano wa kilichotokea katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivi karibuni ambako viongozi kadhaa walifukuzwa akiwamo aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama hicho (UWT), Sophia Simba.
Alisema  aliwahi kutoa angalizo kama hilo kwa vyama vingine kama Tanzania Labour Party (TLP) na Chama cha Demokrasia na Maedeleo (Chadema).


Ngawaiya alivishauri vyama vya siasa  na viongozi wake kabla ya kuchukua hatua za kufukuzana  ni vema kuwaita wahusika ili wajieleze na kutafuta njia nzuri ya kumaliza tofauti ambazo zinakuwa zimejitokeza.
Alisema katika siasa kuna kutofautiana katika mawazo na kupingana, lakini hiyo haina maana ya kujenga chuki na kufikia hata kufukuzana.


“Unapomvua uanachama kada wako, kwanza unapunguza idadi ya wanachama na hawata wale wanaomuunga mkono, hali inayoweza kusababisha chuki na hata visasi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles