25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 4, 2022

Contact us: [email protected]

Cannavaro asalimu amri Yanga

nadir-haroub-cannavaroNa ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM

BEKI wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, ameonekana kusalimu amri ndani ya kikosi hicho baada ya kusema kuwa mabadiliko yaliyopo sasa yanachangia kutopata tena namba kwenye timu hiyo.

Cannavaro ambaye kwa muda mrefu amekuwa majeruhi hali iliyosababisha kutoitumikia Yanga kwenye mashindano ya kimataifa na Ligi Kuu Tanzania Bara yaliyoanza hivi karibuni, nafasi yake hivi sasa imechukuliwa na Andrew Vicent ‘Dante’ pamoja na Vicent Bossou ambao wameonyesha viwango vizuri.

Akizungumza na MTANZANIA Jumamosi, Cannavaro alisema licha ya kutokuwepo kwake kikosini, uwepo wa Dante na Bossou umeonekana kuziba pengo lake, hivyo hana shaka kuwa wataendelea kuitumikia timu kwa mafanikio makubwa.

“Nimekuwa nje kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na majeraha, lakini nashukuru kuona wapo watu walioziba nafasi yangu, tena wanafanya kazi kubwa ndani ya timu, sina shaka kuwa wataendelea kuipa matokeo bora Yanga.

“Binafsi nawaombea Mungu waendelee kuitumikia vizuri Yanga, ili isionekane bila wachezaji fulani timu haiwezi kuwa vizuri, kwani mafanikio ya Yanga ni ya kwetu wote, hivyo majukumu wanayoyatimiza sasa hivi ambayo awali nilikuwa nayo mimi, kutokuwepo kwangu kikosini hakuna madhara yoyote na hivi ndivyo inavyotakiwa,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,544FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles