31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

BUNGE LA ALGERIA KUMUIDHINISHA RAIS WA MPITO LEO

Wabunge wa Algeria wanatarajiwa kumuidhinisha leo rais wa mpito atakayechukua nafasi ya Abdelaziz Bouteflika baada ya rais huyo anayeugua kujiuzulu wiki iliyopita kutokana na maandamano makubwa.

Katiba inasema kuwa Spika wa Baraza la juu la bunge ambaye kwa sasa ni Abdelkader Bensalah mwenye umri wa miaka 77 anastahili kuchukua hatamu za uongozi kwa siku 90 zijazo.

Lakini huku waandamaji wakidai kufanyiwa mabadiliko makubwa mfumo wa kisiasa, utambulisho wa kiongozi wa mpito huenda lisiwe suala ambalo limepata ufumbuzi.

Katika maandamano ya Ijumaa, ya kwanza tangu Bouteflika alipotangaza kuondoka kwake baada ya kupoteza uungwaji mkono wa kijeshi, Waalgeria walidai kuwa viongozi wakongwe wa utawala wa Bouteflika waondolewe kabisa kwenye mageuzi ya kisiasa.

Watu watatu ambao wanalengwa hasa ni spika wa baraza la juu la bunge Bensalah, mkuu wa baraza la kikatiba Tayeb Belaiz na waziri mkuu Noureddine Bedoui.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,625FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles