21 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Klopp aambiwa asiwachukulie poa FC Porto leo

LONDON, ENGLAND

TIMU ya Liverpool leo itarusha karata yake ya kwanza katika mchezo wa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya FC Porto utakaochezwa Uwanja wa Anfield, England.


Katika mchezo huo, kocha wa Liverpool, Jugen Klopp, ameelezwa na mchambuzi pia msaka vipaji wa Kireno katika klabu ya Porto, Tiago Estevao, kuwa anatakiwa kuiogopa timu hiyo hasa wachezaji wawili hatari, Jesus Corona na Moussa Marega.


Mbali na Liverpool, pia mchezo mwingine wa robo fainali utakaochezwa leo, utawakutanisha Tottenham dhidi ya Manchester City katika Uwanja wa Tottenham, England.


Kikosi cha kocha Sergio Coneicao hakijafungwa katika hatua ya makundi, kimeshinda michezo mitano kati ya sita.
Estevao anaamini kuwa uimara huo huenda ukafanya mchezo dhidi ya Liverpool leo ukawa mgumu.


“Kuna wachezaji kadhaa wa kuchungwa na Liverpool katika mchezo huo,” alisema Estevao wakati akihojiwa na gazeti la Express Sprt la England.
“Nyota kama Corona anaonekana kuwa yupo katika msimu mzuri kwenye maisha yake ya soka tangu ajiunge na Porto.


“Ni winga machachari hasa ambaye ni mwiba mkali anapokuwa dhidi ya adui. Ni mchezaji tishio linapokuja suala la kushambulia kwa kushtukiza, pia anafahamu namna ya kuuchezea mpira hivyo si mchezaji wa kawaida kama atacheza eneo hatari dhidi ya Liverpool.


“Ukiachana na nyota huyo hatari, pia Marega ni miongoni mwa wachezaji wa kuogopwa kama Liverpool wakimwachia upenyo watajuta,” alisema Estevao.


Mchambuzi huyo pia aliweka wazi kuwa mashabiki wa Porto wameonekana kuisapoti timu yao kwa kujaa uwanjani kadiri wanavyoweza, hivyo wengi wao watakuwapo leo England.


“Liverpool inaonekana ndio timu inayopewa nafasi ya kushinda leo kama ilivyotokea msimu uliopita, ila wanatakiwa kuwa na tahadhari kwa kuwa mambo mengi yamebadilika,” alisema Estevao.


Wakati huo huo kiungo wa Manchester City, Kevin De Bruyne, amewaonya wapinzani wao, Tottenham kuwa hawaiogopi.


“Sijali kuhusu uwanja wao mpya,” alisema Mbelgiji huyo.”
“Ninachojali ni kuhakikisha tunapata ushindi.

Kila mtu anazungumza kuhusu uwanja wao kama vile ni kitu maalumu kwao, lakini wanachotakiwa kufahamu ni kuwa kila mmoja ana uwanja pia ana watu wa kuwasapoti uwanjani,” aliongeza De Bruyne.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,504FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles