26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

Bunduki za AK 47 zaingizwa nchini kutoka Kenya

Bunduki aina ya AK 47
Bunduki aina ya AK 47

Na Benjamin Masese

SILAHA za kivita zikiwamo za AK 47, SMG na nyingine zimekuwa zikiingizwa nchini kinyemela kutoka Kenya, imeelezwa.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Tarime/Rorya, Justus Kamugisha amesema silaha hizo zimekuwa zikiingia nchini kinyemela kupitia vichochoro ambavyo ni vigumu kuvidhibiti kutokana na mazingira yake.

Ndugu yangu mwandishi suala la hapa mpakani lina changamoto zake… kuhusu silaha kuingia Tanzania kutoka Kenya hilo lipo si kwamba zinangia kwetu la hasha nyingine zinatoka Tanzania kwenda Kenya.

“Tatizo lililopo ni kwamba koo zote zilizopo Mkoa wa Mara zipo Kenya, sasa ni vigumu kumjua huyu ni rai wetu au siyo. Jambo jingine linalosababisha ugumu katika kudhibiti hali hii ni ushirikiano uliopo kati ya raia wa Kenya na Tanzania.

“…yaani huwezi kuwatambua kama ni lugha zote wanazijua, lakini kwa upande wetu wa polisi tumekuwa tukifanya operesheni kila mara na kwa mwezi tunaweza kukamata bunduki mbili hadi nne.

“Changamoto kwetu polisi ni kunyimwa taarifa kutoka kwa wananchi, koo za huku Tarime zina hali ile ya ujasiri na usiri mkubwa. Tunachowaomba wananchi watoe taarifa kwetu kwa sababu silaha hizo ni hatari kwa usalama wao na mali zao,”alisema.

Kamugisaha alisema polisi wanaendelea kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi vya Kenya katika kudhibiti vitendo vya uhalifu mpakani ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kali wale wanaobahatika kukamatwa.

Ametoa kauli hiyo baada ya kuwapo malalamiko ya wananchi juu ya silaha nzito kuingiza nchini kupitia mpakani mwa Tanznaia na Kenya jambo ambalo linawapa wasiwasi ya usalama wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles