24.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

Wakulima walia na taasisi za fedha

Na Fatuma Maumba, Mtwara

BAADHI ya wakulima wa zao la korosho nchini wamesema hawaoni umuhimu wa kuendelea kukopa fedha kutoka katika taasisi za fedha kwa sababu zinawarudisha nyuma kimaendeleo.

Wakulima hao waliyasema hayo walipokuwa wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mkutano ulioandaliwa na Jukwaa la Wadau wa Kilimo Nchini (ANSAF), uliofanyika mkoani hapa na kuwashirikisha wakulima kutoka wilaya mbalimbali zinazolima zao hilo hapa nchini.

Mmoja wa wakulima hao, Tumpale Magehema wa kikundi cha Wakoru Wabanguaji wa Korosho kilichoko wilayani Ruangwa, alisema vyama vya wakulima vinapokopa benki na kushindwa kulipa fedha zilizokopwa wanaokatwa ni wakulima wa korosho jambo ambalo ni kinyume cha utaratibu.

“Wakulima tunaonewa sana wakati korosho ndizo zinazoingiza fedha nyingi hapa nchini na hili linachangiwa na vyama vya msingi vinapokopa fedha benki na kushindwa kuzilipa.

“Wanaposhindwa kulipa fedha zinazokatwa ni fedha zetu sisi wakulima wa korosho ambao hatuna hata hatia kwa kweli tunarudishwa nyuma kimaendeleo kila kukicha.

“Tunasikitika sana kwa tunayofanyiwa kwa sababu hizi taasisi za fedha ziko kibiashara zaidi, yaani hazina mchango wala faida yoyote kwa mkulima mdogo ambaye anahitaji kuwezeshwa,” alisema Magehema.

Naye Oscar Rwechungu wa Benki ya NMB mjini Mtwara, alisema japokuwa wakulima wanaona hakuna manufaa ya kuendelea kukopa kwenye vyombo vya fedha wanatakiwa kujiandaa katika kuendesha maisha yao.

“Mabenki yamekuwa ni mkombozi wa wakulima wa zao la korosho hasa katika mfumo wa stakabadhi za mazao ghalani, kwani wakulima wanaposubiri soko na hawajui mazao yao yatauzwaje hivyo benki zinachukua nafasi ya kuwawezesha kujikimu huku wakisubiri soko.

“Kwa hiyo kama wataona hili haliwafai ni bora watafute njia nyingine za kuendesha maisha yao,” alisema Rwechungu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles