27.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 5, 2023

Contact us: [email protected]

TANESCO, TTCL zahujumiwa Shinyanga

TTCL
TTCL

Na Samwel Mwanga

HUJUMA na wizi wa ndani ya Kampuni ya Simu Tanzania TTCL na transfoma za umeme katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) umeibuka mkoani Shinyanga na kusababisha wananchi kukosa huduma hizo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, viongozi wa taasisi hizo walisema hujuma hizo ilianza Machi na imekuwa ikishamiri kila siku kwa kuibwa nyaya za simu na zaumeme katika maeneo ya mjini na vijijini.

Meneja wa TTCL Shinyanga, Peter Kuguru alisema wizi wa nyaya za simu za mkongo wa chini ulianza mwishoni mwa Machi mwaka huu katika maeneo ya Ngokolo kwa kuibwa nyaya 1,000 hali iliyosababisha eneo la Ikulu ndogo Lubaga kukosa mawasilino ya simu.

Maeneo mengine na nyaya zilizoibwa katika mabano ni Mwasele (300), Chamaguha (50), Viwandani Ugweto (100) na nyaya za juu 50, Kitangiri (50) na Ndala (300) ambazo thamani yake haijajulikana.

Alisema hujuma na wizi huo umekuwa ukiathiri shughuli za kila siku na kusababisha huduma za mawasiliano ya simu za mezani kukosekana pamoja na hasara kwa wenye viwanda hasa vya kuchambua pamba.

Viwanda hivyo ni vya Kisumo Ginnery Ltd, Ahamu Ginnery Ltd, Fresho Investment Ltd, Jambo Group Ltd, GAKI Investment Limited, Afrisian Ginnery Ltd na viwanda vya nguo na ngozi vinavyojengwa na Wachina.

Naye Meneja la TANESCO mkoani Shinyanga, Maugira Gamba alisema hujuma na wizi wa nyaya katika mitambo ya kupoza umeme kutoka njia kubwa ya umeme kwenda kwa wateja umeibuka baada ya transfoma yenye uwezo wa KV 50 iliyokuwa eneo la kijiji Usanda na Kata ya Samuye wilayani Shinyanga.

Alisema Juni 25 mwaka huu watu wasiojulikana walifungua transfoma hiyo juu ya nguzo za umeme na kuishusha chini, wakaibomoa na kuchukua nyaya zote za shaba ndani yamtambo huo.

Alisema kuwa hujuma hiyo imeathiri huduma katika minara ya simu za kampuni za TTCL, Airtel, Zantel na kukatika kwa mawasiliano ya mawimbi ya radio na televisheni zinazorusha matangazo yake kupitia mnara huo wa kituo cha Kilulu katika mlima wa Usanda.

Radio zilizokosa mawasiliano kwa muda ni Radio Free Africa (RFA), Claouds FM na Televisheni ya Star TV yenye makao yake Mwanza.

Gamba alisema kuwa TANESCO imepata hasara ya zaidi ya Sh milioni nane kutokana na hujuma hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles