25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 8, 2024

Contact us: [email protected]

Bulaya awatoa hofu wananchi Bunda

bulayaNa Raphael Okello

MBUNGE wa  Bunda mjini mkoani Mara, Ester Bulaya amewataka  wakazi wa jimbo  hilo  kutokuwa  na wasiwasi kuhusu changamoto  zinazomkabili.

Amesema  yeye bado ni mbunge wao na atatimiza ahadi zake alizowaahidi  wakati wa kampeni za kuwania ubunge mwaka 2015.

Bulaya  aliyasema hayo   kwa nyakati tofauti   alipokuwa akikabidhi jezi   na mpira  kwa timu 23 za mpira wa miguu    Bunda mjini, pikipiki mbili  katika Saccos za vijana ya ‘Ulipo tupo,  Sh milioni moja  kwa Saccos ya akina mama ya Furahisha na  Sh 1,000,000  na viti 20  kwa  Saccos ya Nyasura .

Alisema hiyo ni  miongoni mwa  hatua za kutekeleza  ahadi  ya kuwainua katika uchumi na kuongeza ajira kwa vijana na kina mama.

“Napenda niwahakikishie kuwa mimi bado ni mbunge wenu na nitahakikisha   natimiza ahadi zangu kwenu… nilisema nikiwa muongo katika ujana wangu. Nitakuwa mchawi  nitakapokuwa mzee.

“Hizi fedha ni nje ya fedha ya jimbo, nimezitafuta  kwa njia mbalimbali  lakini pia fedha za jimbo zitakapotoka  pamoja na zile za bajeti ya halmashauri yetu tutapeleka  katika  maeneo yaliyokusudiwa.

“Kwa  mwaka huu pekee mbali na fedha wa mfuko wa jimbo nimetenga  Sh milioni 15   kuongezea nguvu Saccos zilizoko tayari lakini pia nimetumia Sh milioni 12   kwa ajili ya jezi na mipira  kwa timu zote ndani ya jimbo langu,” alisisitiza Bulaya.

Alisema   zipo changamoto  za  maendeleo jimboni humo ikiwa ni pamoja na miundombinu ya barabara, umeme, maji, Elimu na afya na kwamba  atazishughulikia hatua kwa hatua.

Mbunge huyo   hivi sasa anakabiliwa na kesi ya kupingwa   ushindi  wake huku ofisi ya ubunge ikiwa   imempa adhabu ya kutohudhuria  vikao vitano vya bunge.

Akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake kwa mbunge  huyo,  Mwenyekiti wa Saccos ya Nyasura, Samwel Mbasa alisema Bulaya ameonyesha mfano mzuri na kwamba  wako nyuma yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles