27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Askofu awaasa mapadre dhidi ya mashoga

maaskofu-tanzaniaNa Raphael Okello

ASKOFU wa Kanisa la Katoliki jimbo la Bunda mkoani  Mara, Mhashamu Renatus Nkwande amewaasa mapadre wasijinufaishe na fedha za mashoga   kutoka nchi za Ulaya katika kuhamasisha haki za mashoga nchini.

Badala yake aliwashauri  wajishughulishe na kazi ya kuwakomboa katika dhambi.

Askofu alisema hayo juzi katika ibada  maalum ya kumpa daraja Takatifu la Upadre, Shemasi Proper Luhinda iliyofanyika katika viwanja vya Parokia ya Mtume Paulo mjini Bunda.

Alisema   ushoga umeanza kuonekana pia mkoani Mara.

Aliwataka mapadre hao kutekeleza kiapo chao cha utii mbele ya Kanisa   na kwa jamii nzima  kwa  kupiga vita ushoga na aina zote za dhuluma  huku wakiwahubiri jamii  kutunza sheria za nchi na maadili ya Kanisa la Katoliki.

Naye Mkurugenzi wa miito ya Kanisa hilo Jimbo la Bunda, Padre Paulo Kamuhabwa aliwataka vijana  wa kanisa hilo kujiunga na wito wa upadre kwa kuachana na anasa za dunia ili waitumikie jamii popote duniani.

Akisoma kiapo cha utii, Padre huyo mpya aliahidi kutimiza wajibu wake na kuwa na utii na mwadilifu kwa
Askofu wa jimbo hilo, mapadre, watawa na waumini wote.

Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili alilipongeza kanisa hilo kwa utaratibu  uliowekwa wa kuwapata mapadre wema.

Alitoa wito kwa waumini wa kanisa hilo kumuunga mkono Rais Magufuli katika kupiga vita maovu   nchini.

Mwakilishi Msaidizi  wa Baba Mtakatifu nchini Ufaransa, Padre
John Italuma, aliwataka watanzania kutunza amani iiyopo ili  kuepuka ugaidi kama yanayotokea  Ufaransa hivi  sasa kwa kuua watu wasiokuwa  na hatia.

Padre Prosper Luhinda anakuwa wa kwanza kupata daraja Takatifu tangu Jimbo la Bunda lianzishwe miaka mitano iliyopita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles