23.1 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Dk. Mwaka ajisalimisha polisi

DRMWAKANa Veronica Romwald, Dar es Salaam

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linamshikilia tabibu Juma Mwaka wa kituo cha Fore Plan (T) Limited kwa mahojiano baada ya kumsaka kwa siku kadhaa bila mafanikio.

Chanzo cha kuaminika ambacho hakikutaka kutajwa gazetini kwa kuwa si msemaji wa jeshi hilo,  kimeliambia MTANZANIA kuwa tabibu Mwaka alijisalimisha mwenyewe jana kituoni.

“Ni kweli yupo kituoni anahojiwa hadi sasa …. Alijisalimisha mwenyewe mapema hii leo (jana),” kilisema chanzo hicho.

Kilisema tabibu huyo alijisalimisha kituoni hapo ikiwa ni hatua ya kutii wito uliotolewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangwala.

Gazeti hili lilifanya juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Siro kuzungumzia suala hilo hata hivyo simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi haukuweza kujibiwa.

Mapema wiki hii, Dk. Kigwangwala aliliagiza jeshi hilo kumsaka na kumkamata tabibu huyo ndani ya saa 24 huku akimtaka naye kujisalimisha.

Naibu Waziri huyo, alilitaka jeshi hilo kumkamata tabibu huyo mashuhuri kwa kukiuka agizo la serikali lililomtaka kuacha kutoa huduma za tiba asili na tiba mbadala baada ya kufutiwa kibali na Baraza la tiba asili na tiba mbadala.

Baraza hilo lilimfutia kibali tabibu Mwaka baada ya kumkuta hatia ya kukiuka masharti ya sheria ya tiba asili na tiba mbadala ya Mwaka 2002, sheria namba 23, ulaghai wa kujiita daktari na kujifanya amesomea tiba ya kisasa kumbe la.

Aidha katika ukaguzi huo wa kushtukiza alikutwa na shehena ya dawa za kisasa zaidi ya boksi 200 bila vibali vya mamlaka ya chakula na dawa, (TFDA) na kukutwa na shehena ya dawa za tiba asili na tiba mbadala kinyume cha sheria, haswa baada ya kufutiwa usajili wa kutoa huduma hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,718FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles