22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Breaking: Mbowe avamiwa, avunjwa mguu

Mwandishi wetu

Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amejeruhiwa baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo Dodoma.

Taarifa rasmi za awali kutoka kwa ndani ya Chadema na kwa watu wa karibu na Mbowe zinaeleza kwamba tukio hilo lilitokea wakati kiongozi huyo akirejea nyumbani kwake.

Kwa mujibu wa taarifa hizo Mbowe amelazwa katika hospitali moja mjini Dodoma akiendelea na matibabu huku mguu wake mmoja ukiwa umevunjika.

Mtanzania Digital bado ilikuwa ikiendelea kutafuta mawasiliano kutoka ndani ya Jeshi la Polisi mkoani Dodoma ili kupata undani hasa wa tukio hilo.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,502FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles