33.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 19, 2021

Polisi yaeleza Mbowe alivyovunjwa mguu na watu watatu

Mwandishi Wetu

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, amesema kuwa taarifa za awali zinaonyesha Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amevamiwa na watu watatu ambao wamemkanyaga mguu wa kulia na kumvunja.

Akizungumza muda huu Kamanda Muroto, amesema kuwa tayari wameanza uchunguzi wa tukio hilo na atatoa taarifa kamili baadae kwa vyombo vya habari.

“Ni kweli Mbowe amevamiwa na kundi la wahalifu watatu ambao wamemvunja mguu wa kulia na amelazwa katika wodi namba nne Ntiyuka hapa Dodoma.

“Tumeanza uchunguzi na mara baada ya kukamilisha tutatoa taarifa baadae. Hali yake inaendelea vizuri,” amesema Kamanda Muroto

Naye Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, amesema kuwa Mbowe alivamiwa nyumbani kwake kati ya saa sita na saa saba usiku na watu hao.

Alipouliwa hali yake alisema kuwa kwa sasa wanaendelea kufuatilia na watatoa taarifa baadae.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,882FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles