30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

BOT YALILIA UCHUMI WA VIWANDA

NA MWANDISHI WETU – ZANZIBAR


BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imesema ili kuweza kufikia Tanzania ya viwanda, ni lazima jamii ikubali kuunga mkono juhudi za Serikali.

Kutokana na hali hiyo, BoT imesema itaendelea kutoa elimu ya masuala ya uchumi kwa wanahabari ili waweze kujua na kuripoti kwa usahihi taarifa hizo kwa masilahi ya umma.

Kauli hiyo ilitolewa juzi mjini Unguja na Kaimu Mkurugenzi wa Tawi la BoT Zanzibar, Mansour Abdulla.

Alisema BoT imeamua kuendesha mafunzo hayo kwa wanahabari kwa mwaka wa nne mfululizo kama njia ya kuwajengea uwezo wa kuchambua taarifa zinazohusu masuala ya uchumi.

“BoT tunaunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano ya kuwa na uchumi wa kati ambao unatokana na Tanzania ya viwanda. Ni imani yangu kwamba mafunzo haya yatachochea kuandika na kuchambua namna bora ya kuhamasisha Watanzania na wawekezaji wa nje kuja kuona fursa tulizonazo nchini kwetu.

“Ikiwa kila mmoja atatimiza wajibu wake kwa kufanya kazi na kuchochea maendeleo, ni wazi ndoto ya Rais Dk. John Magufuli ya kuwa na Tanzania ya viwanda itafanikiwa, kwa kuwa hivi sasa kuna idadi kubwa ya watu walioomba kuja kuwekeza hapa nchini,” alisema Mansour.

Pamoja na hayo, aliwaahidi waandishi kwamba ataendelea kutoa mafunzo hayo kila mwaka ili kuhakikisha habari za uchumi na fedha zinaandikwa na kuripotiwa na kuifikia jamii kwa ufasaha zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles