BOCCO AWAPA MKONO WA MWAKA MPYA MASHABIKI AZAM

0
943

NA MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


john-boccoNAHODHA wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, John Bocco, amewatakia mashabiki wa timu hiyo heri ya mwaka mpya 2017, huku akiwashukuru kwa sapoti yao waliyoionyesha mwaka huu.

Bocco ametoa kauli hiyo hivi karibuni, mara baada ya kumalizika kwa mchezo uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons, walioifunga bao 1-0, huku akifanikiwa kutupia bao hilo pekee lililorudisha morali ndani ya kikosi hicho baada ya kutofanya vizuri kwenye mechi mbili za ufunguzi wa mzunguko wa pili walipocheza ugenini na African Lyon (0-0) na Majimaji (1-1).

“Kwanza tunawashukuru mashabiki wetu kwa uvumilivu waliouonyesha, kwa sapoti waliyotupa katika kipindi chote kigumu tulichopitia, kama wachezaji na timu kwa ujumla, tunawaomba waendelee kuwa na moyo huo huo na pia tunawatakia heri ya mwaka mpya (2017) na wamalize mwaka huu vizuri, tuendelee kuwa pamoja ili kuisaidia timu yetu iweze kufanya vizuri,” alisema Bocco.

Bocco, ambaye ameipatia mafanikio makubwa Azam FC kwa mabao yake muhimu tokea timu hiyo ikiwa madaraja ya chini hadi kupanda Ligi Kuu mwaka 2008, alisema kuwa wamepitia changamoto nyingi sana kwa mwaka huu unaokwisha, huku akidai kuwa, wamejifunza kupitia hayo na wanachoangalia kwa mwaka mpya ni kuipeleka mbele zaidi timu hiyo ili kufikia mafanikio.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here