25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

TFF KUTENDA HAKI SUALA LA MCHEZAJI VENANCE LUDOVICK

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


 

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limeahidi kutenda haki kuhusiana na mchezaji wa African Lyon, Venance Ludovick, huku likiwataka wadau wa mchezo huo nchini kupuuza taarifa za kwenye mitandao kuhusu mchezaji huyo.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, alisema Dar es Salaam jana kuwa, suala la mchezaji huyo linaendelea kufanyiwa kazi na Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji.

“Tunawahakikishia umma wa wapenda soka nchini kuwa haki itatendeka kwa mujibu wa kanuni zinazoendesha mashindano husika,” alisema Lucas.

Mchezaji huyo analalamikiwa na timu ya Yanga kwa kucheza katika mechi yao dhidi ya African Lyon iliyochezwa Desemba 23, mwaka huu katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara kufungana bao 1-1, huku kwa Lyon bao lao likifungwa na mchezaji huyo.

Hata hivyo, mara baada ya mechi hiyo, timu ya Yanga ilikata rufaa katika Kamati hiyo ikitaka timu hiyo ipokwe ushindi kutokana na kumchezesha mchezaji huyo, ikidai kuwa hakukamilisha taratibu za usajili kutoka katika timu ya Mbao FC ya Mwanza na kwamba bado alikuwa na mkataba wa kuichezea timu hiyo.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa African Lyon, Ernest Brown, alitoa ufafanuzi kuwa mchezaji huyo alijiunga na timu hiyo akiwa mchezaji huru, hivyo hakuna haja ya wao kutaka malumbano.

Mchezaji huyo alinukuliwa akisema kuwa aliandika notisi ya saa 24 ya kuvunja mkataba na timu ya Mbao FC Desemba 13, 2016, kutokana na kutolipwa mishahara yake ya miezi minne na fedha za usajili, Sh 3,500,000 ambazo Mbao FC ilishindwa kumlipa.

Timu za Mbao na Yanga zinapinga mchezaji huyo kuichezea African Lyon akiwa mchezaji halali wa Mbao, aliyoichezea mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kwa mujibu wa vielelezo vilivyowasilishwa na Mbao FC, inadaiwa Ludovic alihamia Mbao FC kimakosa na akatumika kimakosa pia, hivyo Yanga inaweza kushinda rufaa hiyo na kuvuna pointi mbili zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles