25.6 C
Dar es Salaam
Friday, December 2, 2022

Contact us: [email protected]

BLAC CHYNA ALITAKA GARI LAKE KWA ROB

LOS ANGELES, MAREKANI

ALIYEKUWA mke wa Rob Kardashian, Blac Chyna, ameweka wazi kuwa analitaka gari lake aina ya Range Rover ambalo alimpa zawadi baba wa mtoto wake.

Blac alionesha jeuri ya fedha kwa kununua gari hilo toleo la mwaka 2016 na kumkabidhi baba wa mtoto wake Rob kama zawadi, lakini baada ya kuachana na mrembo huyo, anaomba kurudishiwa gari hilo, lakini Rob anakataa.

Si mara ya kwanza Blac kumpa gari Rob, awali alimpa gari aina ya Ferrari na Lamborghini, lakini magari hayo walikuwa wanayatumia wote, ila Range Rover alimpa moja kwa moja kama zawadi, ila baada ya kuachana miezi miwili iliyopita mrembo huyo amedai anataka gari yake.

Rob anakataa kutoa gari hiyo, lakini familia yake inatarajia kukutana kesho ili kutaka kumshawishi alirudishe gari hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,504FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles