25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, September 28, 2023

Contact us: [email protected]

KYLIE: SINA UGOMVI NA TYGA

LOS VEGAS, MAREKANI

MWANAMITINDO maarufu nchini Marekani, Kylie Jenner, amefunguka kwa mara ya kwanza na kusema kuwa hana ugomvi wowote na aliyekuwa mpenzi wake rapa Micheal Stevenson ‘Tyga.’

Wawili hao walikuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu, lakini miezi michache iliyopita mrembo huyo alitangaza kuachana na Tyga na sasa anatoka na rapa Travis Scott.

Kwenye akaunti ya Instagram, Kylie ameweka wazi kuwa kuachana na Tyga kulikuwa kwa amani na wala hawana tatizo lolote hadi sasa.

“Sina tatizo na Tyga, nilifanya maamuzi ya kuachana naye kwa kuwa ninaamini mimi ni mdogo sana na bado nina nafasi kubwa ya kufanya mambo mengi kwa ajili ya maisha yangu, hivyo tulifikia makubaliano mazuri, bado tunawasiliana kwa kuwa hatuna ugomvi wowote kati yetu.

“Kwa sasa siwezi kuangalia mambo ya miaka mitano yaliyopita, natakiwa kuangalia mambo makubwa ya kufanya miaka ijayo,” alisema Kylie.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,750FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles