23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

BAKWATA YATANGAZA SIKU YA SIKUKUU YA EID EL HAJJ KUWA SEPTEMBA MOSI

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limeutangazia umma wa Tanzania kuwa sikukuu ya EID-EL-ADHAA (Eid ya kuchinja) itakuwa tarehe 1 Septemba, 2017 Siku ya Ijumaa.

Kwa mujibu wa Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Zubeir Ally, amethibitisha mwandamo wa mwezi na kwamba siku ya Agosti 31 ni siku ya kufunga sunna ya Arafa, wakati Septemba Mosi ni sikukuu.

Mufti Zubeir ameeleza kuwa kitaifa sikukuu hii itaadhimishwa mkoani Dar es Salaam na Swala ya eid itaswaliwa katika uwanja wa Garden, nyuma ya Msikiti wa Taqwa uliopo Ilala Bungoni pia Baraza la Eid litafanyika mara baada ya swala ya Eid eneo hilo hilo.

Katika hilo, Mufti amewatakia waislamu wote na nchi kwa Ujumla Eid el-adh-ha njema pamoja na kuwasihi kutumia kipindi hiki cha mwisho wa mwaka wa kiisilamu (1438) kutafakari maadili mema ndani ya jamii itakayokuwa bora nay a kupendana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles