23.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

BIRDMAN AMVISHA TONI PETE YA UCHUMBA

NEW YORK, MAREKANI


HATIMAYE rapa Bryan Williams ‘Birdman’, amemvisha pete ya uchumba mpenzi wake wa muda mrefu, Toni Braxton (50) wakati wa kipindi cha runinga cha reality TV show.

Toni ni staa wa muziki pamoja na vipindi vya runinga nchini Marekani, hivyo juzi alishtukizwa na mpenzi wake Birdman na kumvisha pete hiyo wakati anaendesha vipindi vyake.

Birdman (49) amekuwa akihusishwa kutoka kimapenzi na mrembo huyo, lakini alikuwa anakanusha, ila rapa huyo ameamua kutuliza kelele hizo za mashabiki kwa kuamua kuvunja ukimya huo.

Toni hadi sasa ana watoto wawili, wa kiume Denim mwenye umri wa miaka 16 na Diezel mwenye miaka 14, watoto hao aliwapata huku akiwa na msanii mwenzake, Keri Lewis. Wawili hao walifunga ndoa mwaka 2001 na wakaja kuachana mwaka 2009.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles