23.8 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

RIHANNA: USIMWAMINI MTU CHINI YA MIAKA 30

NEW YORK, MAREKANI


NYOTA wa muziki wa Pop nchini Marekani, Robyn Fenty ‘Rihanna’, juzi alikuwa anasherehekea kutimiza miaka 30 ya kuzaliwa, hivyo alitumia akaunti yake ya Instagram na kusema ‘usimwamini mtu chini ya miaka 30’.

Mrembo huyo alikuwa na maana kwamba watu wenye umri chini ya miaka 30 wamekuwa na maamuzi tofauti, hivyo si watu wa kuwaamini katika maisha.

“Ninakumbuka mengi ambayo nilikuwa nayafanya wakati wa umri wa miaka 20, lakini sasa nina furaha kubwa kwa kuwa nimefikisha miaka 30, huu ni umri ambao unaweza kufanya jambo na ukaaminika kwa kila mtu. Sasa naweza kusema nimefikia utu uzima, namchukia Rihanna yule wa chini ya miaka 30,” aliandika Rihanna.

Mashabiki wa msanii huyo walitumia mitandao ya kijamii kumpongeza kwa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na kufikisha miaka 30.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,248FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles