26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

BIEBER, SELENA WATIKISA JAMAICA

KINGSTON, JAMAICA


STAA wa muziki nchini Marekani, Justin Bieber na mwanamitindo maarufu Selena Gomez, mapema wiki hii walikuwa nchini Jamaica kwenye sherehe ya harusi ya baba wa Bieber.

Wawili hao miezi ya hivi karibuni wamekuwa wakitajwa kuwa wamemaliza tofauti zao na sasa wamerudi kwenye uhusiano kama ilivyo awali.

Kwa kuthibitisha hilo, baba wa Bieber alitumia ukurasa wake wa Instagram kuposti picha ya wawili hao wakiwasili kwenye uwanja wa ndege nchini humo kwa ajili ya kusherehekea harusi hiyo.

Picha hiyo ilileta gumzo kubwa kwa mashabiki wa msanii huyo ambaye mwaka jana alikuwa anatamba na wimbi wake wa ‘Sorry’ pamoja na ‘What do you Mean’.

Tayari baba wa Bieber mwenye umri wa miaka 42, amefanikiwa kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu, Chelsey Rebelo mwenye umri wa miaka 29. Mbali na Beiber na Selena kualikwa kwenye harusi hiyo, wengine ni pamoja na Dr. Rita Kilislian na Taylor Smith.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles