26.5 C
Dar es Salaam
Friday, January 28, 2022

Bilo awafungia kazi washambualiaji Alliance

NA MOHAMED KASSARA-DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Alliance FC, Athumani Bilal ‘Bilo’ amesema licha ya kuridhishwa na kiwango kilichooneshwa na vijana wake katika michezo ya kirafiki waliocheza, atatumia muda mchache uliobaki kuongezea makali safu ya ushambulaji kabla ya kuivaa Mbao FC.

Alliance inatarajia kucheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara Agosti 24, mwaka huu dhidi ya Mbao FC, Uwanja wa Kirumba, Mwanza.

Timu hiyo imetoka kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya  Pamba,  inayoshiriki Ligi  Daraja Kwanza (FDL) na kulazimishwa sare ya bao 1-1, wiki iliyopita.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Bilo alisema kuwa amefurahishwa na viwango vya wachezaji, lakini atalazimika kusuka upya safu ya ushambuliaji kwa ajili kuhakikisha inafunga mabao mengi.

“Ni kweli kabisa vijana wangu wapo katika kiwango bora, wanacheza kwa ushirikiano mkubwa na kila mmoja ana morali ya juu, hali hii inanipa imani kuwa tutakuwa na msimu mzuri.

“Lakini kabla ya kucheza na Mbao, nitaisuka upya safu ya ushambualiaji ili iweze kutumia nafasi zinazopatikana, mpango huo ukikamilika usishangae kusikia tukimpiga nyingi, kwani vijana wako moto sana,”alisema Bilo.  

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
177,106FollowersFollow
532,000SubscribersSubscribe

Latest Articles