23.6 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Bares afichua siri ya kambi Zanzibar

NA MOHAMED KASSARA – DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa timu ya JKT Tanzania, Abdallah Mohamed ‘Bares’ amefichua kuwa,  kambi yao waliyoiweka visiwani Zanzibar ni mahususi kwa ajili ya kuhakikisha wanauanza vema msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kwa  kupata matokeo chanya dhidi ya Simba.

JKT Tanzania inatarajia kukata utepe wa Ligi Kuu Tanzania Bara Agosti 29, mwaka huu kwa kumenyana na mabingwa hao watetezi wa taji hilo, Simba, mchezo utakaochezwa Uwanja wa Meja Jenerali Michael Isamuhyo, Dar es Salaam.

Katika kuhakikisha inafanya vema katika mchezo huo na mingine, kikosi cha Maafande hao wa Jeshi la Kujenga Taifa, kimejichimbia Zanzibar, kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi hiyo.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Bares alisema  kikosi chake kimeendelea kujifua vikali kwa ajili ya kuhakikisha kinaanza msimu mpya kwa kupata pointi zote tatu katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Simba.

Alisema anafahamu umuhimu wa kupata ushindi katika mchezo wa kwanza wa ligi, hivyo atahakikisha anawandaa kikamilifu vijana wake kuvuna pointi tatu au moja, lakini si kutoka patupu.

“Maandalizi yetu kuelekea msimu mpya yako vizuri na kadri siku zinavyozidi kwenda tutazidi kuwa imara, vijana wote wapo katika hali nzuri, pia tunashukuru  hatuna majeruhi.

“Tumejiandaa kufanya vizuri msimu ujao, tutahakikisha tunakwenda zaidi pale tulipoishia, tunajua tunafungua msimu kwa mchezo mgumu dhidi ya Simba, lakini tutahakikisha hatupotezi pointi tatu katika mchezo huo, tumejipanga kuanza vizuri ligi, hivyo ni muhimu kuanza kwa kupata matokeo chanya,”alisema kocha huyo wa zamani wa Tanzania Prisons.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,070FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles