25.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Bandari Dar yakanusha kuchelewesha sukari

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Bandari ya Dar es Salaam imekanusha taarifa zinazosambaa ikidaiwa kuchelewesha mzigo katika bandari hiyo ikiwamo sukari.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Bandari hiyo, Mrisho Mrisho leo Februari 4,2024 jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari.

Mrisho amesema shughuli za kutoa mzigo bandarini zinaendelea kwenye gati zote na zipo meli zinashusha mizigo masaa 24.

Amesema kuanzia Februari 1 hadi 4 wamehudumia zaidi ya meli 10 na tatu zimeondoka leo baada ya kushusha mizigo, hivyo amewahakikishua kuwa bandari inafanyakazi.

“Sio kweli kwamba mzigo hautoki bandarini mtu lazima awe amekamilisha taratibu zote ndio mzigo utoke na ndani ya bandari kuna taasisi 30 zinafanyakazi, aseme ni taasisi gani imekwamisha mzigo usitoke,”amesema Mrisho.

Kuhusu sukari ameeleza kuwa walipokea barua ya ombi kutoka Bodi ya Sukari wafanyie kazi meli tatu zenye sukari kwa kutoa haraka.

“Tumepokea ombi hili sisi bandari tumefanyia kazi tayari kwa sababu ni mahitaji muhimu, mzigo wa sukari unahitajika sokoni sisi tumetekeleza jukumu hili la kutoa sukari kwenye meli hizo,” ameeleza.

Mrisho amesema kipindi cha nyuma kwa mwezi walikuwa wanahudumia tani milioni 1. 6, kwa sasa wanahudumia tani milioni 2.5 kwa mwezi na wanahitaji kuvuka zaidi.

Amesema kwa upande wa kontena au kasha kipindi cha nyuma walikuwa wanahudumia 50,000 kwa mwezi kwa sasa ni zaidi ya 90,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles