32.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 20, 2024

Contact us: [email protected]

Brela yahimiza wadau kusajili alama za bidhaa, huduma

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) umewataka wananchi kusajili alama za biashara na huduma ili kuendesha shughuli zao kihalali na kunufaika na fursa mbalimbali za kiuchumi zinazopatikana katika mfumo rasmi.

Akizungumza Januari 29,2024 kwenye Maonesho ya Wiki ya Sheria katika uwanja wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Ofisa kutoka kitengo cha Miliki Bunifu Brela, Ulumbi Kullian, amesema kusajili alama ya bidhaa na huduma kunasaidia kuzipa biashara uhai wa kisheria.

Amesema wafanyabiashara wengi wamekuwa wakiendesha shughuli zao na kutumia alama bila kuzisajili hatua inayosababisha wakati mwingine kusajiliwa na watu wengine.

“Alama za bidhaa na huduma zinatofautisha bidhaa moja na nyingine, kwahiyo mtu akisajili inasaidia kumlinda yeye na bidhaa yake na mtu mwingine hataweza kutengeneza kitu kinachofanana nacho.

“Tumekuwa tukitoa elimu katika maeneo mbalimbali kama hivi kwenye maonesho ambayo imesaidia kuhamasisha jamii kuja kusajili alama za biashara.

“Tunawashauri ambao wanatumia majina bila kuyarasimisha wafike kwetu wajisajili na kurasimisha alama zao za biashara na huduma ili kunufaika na fursa mbalimbali za kiuchumi zinazopatikana katika mfumo rasmi,” amesema Ulumbi.

Wakala huo unatumia maonesho hayo kutoa huduma za usaidizi kwa wadau waliopata changamoto katika shughuli za biashara na waliokwama kujisajili kwa njia ya mtandao.

Pia unatoa huduma za papo kama vile za usajili wa majina ya biashara, kampuni, utoaji wa leseni za biashara kundi A na usajili wa viwanda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles