26.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Wanaume Temeke waanza kushuhudia wake zao wakijifungua

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Hospitali ya Rufaa Mkoa Temeke (TRRH) imeanza rasmi kutoa huduma ya kujifungua ukiwa na msaidizi yaani mama, mwenza au dada na kuruhusu mama anayejifungua kuchagua muuguzi anayemtaka kama muongozo mpya wa chati uchungu unavyosema.

Maboresho hayo yamefanywa ili kumwezesha mama mjamzito kupata huduma bora zaidi na kuwa karibu na msaidizi wake pamoja na kuzingatia utu na heshima kwa mama mjamzito.

Hassan Mwauta mkazi wa Chamazi ambaye ni mume wa mmoja wa wajawazito waliotumia huduma hiyo katika hospitali hiyo ameipongeza Serikali kwa maboresho hayo.

Mkazi wa Chamazi, Hassan Mwauta.

“Nilimleta mke wangu kuja kujifungua katika hospitali ya Temeke, nilisikia kuna huduma ya mzazi kujifungua akiwa na mwenza wake na nilipofika nimejionea mwenyewe, nimeshangaa kwa kweli mazingira ni mazuri na huduma ni nzuri, unaweza kuingia na mjamzito wako ukakaa naye muda wowote unaotaka,” amesema Mwauta.

Naye Ofisa Mkunga katika hospitali hiypo, Shukrani William, amesema wodi ya kujifungulia kina mama imeboreshwa na kwamba huo ni moja ya mikakati ya kuunga mkono jitihada za serikali kuhakikisha sekta ya afya inaboresha huduma na kuboresha maisha ya mama na mtoto wakati wa kujifungua.

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke inaendelea kufanya boresho ya miundombinu ili kutoa huduma bora zaidi kwa Watanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles