27.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Kinana: Sheria ya uchaguzi imekidhi mahitaji ya Kimataifa na Afrika

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Bara, Abdulrahaman Kinana amesema sheria ya uchaguzi iliyopitishwa na Bunge hivi karibuni imekidhi mahitaji ya Kimataifa na Afrika.

Hayo ameyabainisha leo Feburuari 4,2024 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam wakati akihutubia mkutano wa wanachama wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam.

Amesema wanachama wa chama hicho wajipange kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu.

“Sheria ya Uchaguzi iliyopitishwa na Bunge ni nzuri kuliko sheria nyingine zote ambazo tumekuwa nazo katika chaguzi zetu tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1995. Niwasihi Watanzania na vyama vya siasa tuikubali sheria hii ambayo imekubali mapendekezo mengi yaliyotolewa na wadau.Ni sheria ambayo imepunguza hata mamlaka ya Rais kwa mfano sheria hii inaeleza wazi Rais hatakuwa na mamlaka ya kuteua mwenyekiti pamoja na makamu mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na badala yake atapelekewa tu mapendekezo.

“Wakurugenzi wa halmashauri hawatakuwa wasimamizi wa uchaguzi na badala yake sheria hiyo inaeleza watumishi wa umma wenye uzoefu na kwa sifa zao ndio watakaopewa nafasi hiyo, hakika sheria hii ni nzuri kuliko sheria zote ambazo zimekuwa zikitumika katika uchaguzi,” amesema Kinana.

Vilevile amewaomba wana Chadema na watanzania wamuunge mkono Rais Samia kwani ana dhamira nzuri na Taifa hili hakuna sababu ya kuandamana.

Akizungumzia maridhiano ambayo yamefanyika kwa nyakati tofauti, Kinana amesema kuwa wakati Rais Dk.
Samia Suluhu Hassan anaingia madarakani kulikuwa na wanachama wa CHADEMA wasiopungua 400 wako mahabusu wakikabiliwa na kesi zilizotokana na sababu mbalimbali za kiuchaguzi,lakini ulitengenezwa utaratibu kupitia taratibu za kisheria na nwanasheria mkuu wote waakachiwa.

Amesema kwa nia njema ya Rais Samia Serikali ilikubali kuwalipa CHADEMA sh bilioni 2.7 za ruzuku kwa miaka mitatu ambayo walikataa kwa kugomea matokeo ya uchaguzi mkuu mwaka 2020.

“Rais Dk.Samia aliagiza Serikali kuwalipa chadema ruzuku hiyo ili kulinda maridhiano.Pamoja na kulipwa fedha hizo CHADEMA hawajawahi kusema kama wamelipwa au kusema ahsante, wamekaa kimya,” ameeleza.

Amesema ukweli usiposemwa na upotoshaji unageuka kuwa kweli, hivyo halikubaliki pamoja na matatizo mengi ikiwemo ya kiuchumi na kijamii lakini yanashughulikiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles