BALOZI WA MAREKANI AJIUZULU KUPINGA SERA ZA TRUMP

0
592

WASHINGTON, MAREKANI


MWANADIPLOMASIA wa cheo cha juu wa Marekani nchini China, amejiuzulu katika kile kinachoonekana kutokubaliana na sera za mabadiliko ya hali ya hewa za Rais Donald Trump.

Vyombo vya habari nchini hapa vilisema kuwa Naibu Balozi, David Rank alijiuzulu kufuatia tangazo la Trump wiki iliyopita kuwa Marekani ilikuwa inajiondoa kutoka kwa makubaliano ya Paris.

Hatua hiyo ambayo Trump alisema kuwa itasaidia kulinda uchumi wa Marekani, ilizua hisia tofauti kote duniani.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema katika taarifa yake kuwa Rank alifanya uamuzi binafsi.

Rank ambaye aliteuliwa Januari mwaka jana, alikuwa mwanadiplomasia mkuu wa Marekani nchini China kwa kuwa alikuwa kaimu Balozi.

Terry Branstand ambaye aliteuliwa na Trump, atachukua wadhifa huo.

Rank alianza kutumikia wadhifa huo mwaka 1990 na ameshatumikia nchini Afghanistan, Taiwan, Ugikiri na Mauritius.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here