23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

DC: WANAOJIRI  WATOTO MIGODINI WAKAMATWE

Na RAPHAEL OKELLO


MKUU wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili, ameliagiza jeshi la polisi kuwakamata na kuwafikisha mahakamani wazazi na walezi ambao watoto wao wanajihusisha na ajira   migodini.

Alisema lengo ni  kukomesha uvunjaji wa haki za watoto.

Akizungumza na wachimbaji wa Kijiji cha Kamkenga jana, Bupilipili alisema agizo hilo linahusisha   wamiliki wa migodi ambao wamekuwa na tabia ya kuwaajiri watoto na kuwatumikisha biashara au kufanya kazi mbalimbali za ndani badala ya kuwapeleka shule.

“OCD nakuagiza kuanza sasa mtoto yeyote atakayepatikana mgodini akifanya kazi mkamate ili amtaje  mzazi wake naye akamatwe.

“Lakini aliyempa ajira hiyo naye hakikisheni anakamatwa kwa sababu   wanawachochea watoto kuacha shule  na kujiingiza katika biashara hizi,” alisema Bupilipili.

Alisema mtoto anapaswa kusoma shule na siyo ajira, hivyo haiwezekani wazazi kuwatumikisha watoto ili wapate riziki kwa kisingizio cha hali ngumu ya maisha.

DC alisema watoto  hata wakiwa kwenye ajira hawana uwezo kujadiliana  na mwajiri kupata malipo stahiki lakini pia ni kinyume na sheria.

  Bupilipili  pia alitangaza kufunguliwa  mgodi  wa Kamkenga ambao ulifungwa kwa takribani wiki moja kupisha  ukaguzi wa usalama  wa mgodi.

Alisema  shughuli  za uchimbaji ziliruhusiwa katika  maduara 22 yaliyothibitishwa  kuwa  salama na mengine 44 yakiagizwa kufanya marekebisho kadhaa  kabla ya serikali kuruhusu shughuli hizo kuendelea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles