23.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 10, 2022

Aussems kama Zahera

NA MOHAMED KASSARA-DAR ES SALAAM

HATIMAYE Klabu ya Simba imefikia uamuzi wa kuachana na aliyekuwa Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Patrick Aussems aliyedumu kwenye kikosi hicho kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu.

Uamuzi huo  umekuja baada siku tano kupita,  tangu kocha huyo aliposimishwa kazi na kuitwa na kikao cha Bodi ya Wakurugenzi ya klabu kutokana na makosa ya kinidhamu.

Aussems alijiunga na Simba Julai mwaka jana na kusaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia timu hiyo, akirithi mikoba iliyoachwa na Mfaransa Pierre Lechantre.

Mbelgiji huyo  anaondoka Simba akiwa amekiongeza kikosi hicho kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita  na kuifikisha hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kocha huyo anaondoka na rekodi ya kukiongoza kikosi hicho kucheza mechi 48 za Ligi Kuu Tanzania Bara, akishinda 44 na kupoteza nne.

Tangu msimu huu uanze, Aussems alikuwa ameifundisha Simba katika michezo 10 ya ligi na kuvuna pointi  25  , ikishinda nane , sare moja na kupoteza idadi kama hiyo.

Aussems sasa ataungana na kocha wa zamani wa watani zao, Yanga,  Mwinyi Zahera aliyetimuliwa na klabu hiyo Novemba 5, mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa jana na uongozi wa Simba kupitia kwa Afisa Mtendaji Mkuu, Senzo Mazingiza ilisema kuwa, klabu hiyo imefikia uamuzi wa kusitisha kibarua cha kocha huyo kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu kwa kiwango na malengo aliyopewa.

Alisema kocha huyo alishindwa kufikia malengo ya kuipeleka timu hiyo katika hatua ya makundi ya Ligi Mabingwa Afrika msimu huu, lakini pia kushindwa kujenga timu yenye ari ya mafanikio na nidhamu.

“Maelezo yaliyotolewa na kocha huyo Novemba 28, mwaka huu hayakuiridhisha, Kamati ya Nidhamu dhidi ya tuhuma za kuondoka bila ruhusa ya klabu, ikizingatiwa kocha huyo alikataa kuiambia kamati sehemu alipokwenda na sababu.

“Mchakato wa kumpata mrithi wake umeanza mara moja, Bodi imemchagua Dennis Kitambi kukaimu nafasi hiyo hadi pale kocha Mkuu mpya atakapopatikana , “ilieleza taarifa hiyo ya Mazingiza.

SSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSS

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,395FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles