27 C
Dar es Salaam
Friday, May 27, 2022

Auawa na baba yake baada ya kuchelewa kurudi nyumbani

YOHANA PAUL Na BENJAMIN MASESE, MWANZA

BINTI mmoja mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Kayenze, Kata ya Kayenze Wilaya ya Ilemela mkoani hapa, Veronica Anthony (17), amefariki dunia huku ikidaiwa sababu ni kupigwa na kitu kizito kichwani na baba yake mzazi, Anthony Costantine (50) kwa kosa la kuchelewa kurudi nyumbani.

Akizungumuzia tukio hilo jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro, alidai tukio hilo lilitokea Septemba 8 mwaka huu majira ya saa nne usiku ambapo mtuhumiwa ambaye ni baba mzazi wa marehemu alimpiga na kitu kizito kichwani binti yake kutokana na kukasirishwa na kitendo cha binti huyo kukawia kurejea nyumbani.

Muliro alisema mtuhumiwa huyo amekamatwa na atafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria na mwili wa marehemu umehifadhiwa hopitali ya Rufaa ya Bugando kwa uchunguzi wa daktari.

Aidha jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza linamushikilia Mussa Gabriel (35), kwa tuhuma za kumuua ndugu yake Emmanuel Joseph (49) wakiwa eneo la Mhonze A, Kata ya Shibula Wilaya ya Ilemela mkoani hapa.

Kamanda alisema chanzo cha tukio hilo inadaiwa marehemu alikuwa akimtuhumu mtuhumiwa kumwibia simu yake ya mkononi aina ya tecno ya batani yenye thamani ya Sh 40,000.

Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya Sekou-Toure kwa uchunguzi wa daktari.

Pia Jeshi la Polisi mkoani hapa linamsaka mtu mmoja anayefahamika kwa jina moja la Anthony, Mkazi wa Mabuki Wilaya ya Kwimba kwa tuhuma za kubandua na kulichana kwa makusudi bango lenye picha ya mgombe ubunge Jimbo la Kwimba, Sharifu Mansoor kinyume cha sheria na mtuhumiwa atakapokamatwa atafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,454FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles