27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi 92,940 wapambania nafasi 54,000 za mikopo elimu ya juu

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imefunga dirisha la maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao kwa mwaka wa masomo 2020 wakati ikiwa wanafunzi 92,947 wameshaomba huku wanaotarajiwa kupata mkopo wakiwa ni 54,000.

Taarifa kwa umma iliyotolewa jijini Dar es Salaam jana na kusainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa (HESLB), Abdul-Razaq Badru, ilisema mfumo wa maombi hautaweza kuruhusu usajili wa maombi mapya ya waombaji isipokuwa kwa waombaji 7,500 waliopo mtandaoni ambao hawajakamilisha maombi hayo.

Badru alisema HESLB ilifungua dirisha la maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao kwa siku 40 kuanzia Julai 21.

Alisema kufuatia maoni na maombi ya wazazi, walezi na wanafunzi, tume iliongeza muda wa siku 10 hadi zilizokamilika jana.

 â€œLeo (jana) saa 6:00 usiku dirisha la upokeaji wa maombi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2020/21 kwa njia ya mtandao litafungwa rasmi. Baada ya muda huo, usajili mpya kwa ajili ya maombi mapya hautaruhusiwa,’’ alisema Badru

AIdha, Badru alisema Oktoba Mosi HESLB itaanza zoezi la uchambuzi wa maombi hayo na baadaye itaorodhesha maombi yote yenye mapungufu na kuwatangazia waombaji husika kwa ajili ya kurekebisha kasoro zilizojitokeza.

Badru aliwataka wazazi, walezi na wanafunzi kuendelea kufuatilia vyanzo rasmi ikiwemo tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz) kuhusu taarifa muhimu na orodha ya watakaopangiwa mikopo kwa mwaka wa masomo 2020/2021 kwa mujibu wa kalenda ya mwaka wa kitaaluma (academic almanac) ya mwaka huu.

Serikali kupitia HESLB, imetenga Sh bilioni 464 kwa ajili ya wanafunzi 145,000, ambapo kati yao wanafunzi wanufaika 54,000 watakuwa wa mwaka wa kwanza na 91,000 ni wanaoendelea na masomo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles