30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Luis, Mugalu waongeza nguvu Simba

NA ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM

KIKOSI cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba, kimewasili mkoani Morogoro jana kikiwa na matumaini kibao baada ya nyota wao watano waliokosekana katika mchezo uliopita, kurejea kundini tayari kuivaa Mtibwa Sugar kesho.

Wekundu wa Msimbazi hao wanatarajiwa kushuka dimbani kuumana na Mtibwa Sugra katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini humo.

Simba ilizindua vema kampeni zao za kutetea taji lao kwa kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu katika mchezo uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Katika mchezo huo, Simba ilikosa huduma za nyota wake, Gerson Fraga aliyekuwa na matatizo ya kifamilia, Ibrahim Ame na Chris Mugalu waliokuwa wanasumbuliwa na majeraha, huku Luis Miquissone na Pascal Wawa, hawakuwa na utimamu wa mwili (fitness).

Akizungumza na MTANZANIA jana, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu, alisema wachezaji hao ni miongoni mwa wakali 28 waliounda kikosi kilichokwenda Morogoro na kuna uwezekano mkubwa wakapata nafasi ya kucheza kutokana na kuwa fiti.

“Wachezaji watano ambao hawakuwepo katika mechi iliyopita, wote wapo vizuri na tumeambatana nao kuelekea Morogoro, kazi ni kwa kocha kuamua kuwatumia au la, lakini hawana tatizo lolote kwa sasa,” alisema.

Wakati Rweyemamu akisema hayo, Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vanderbroeck, amesema kuwa msimu huu anahitaji idadi kubwa ya mabao kupita ule uliopita na jukumu kubwa alilowapa wachezaji wake ni kufunga mara mbili ya kila mechi waliyocheza awali.

“Msimu uliopita tulimaliza ligi tukiwa na mabao 78, ni mengi ukilinganisha na timu nyingine, msimu huu nahitaji idadi hiyo iongezeke, ndio maana nimeomba kuboreshewa safu ya ushambuliaji, lakini pia kila mchezaji anayepata nafasi ya kufunga, anatakiwa kufanya hivyo.

“Malengo yetu ya ubingwa ili yatimie, lazima tupate matokeo ya ushindi wa pointi tatu kwenye mechi zetu zote, lakini msingi mkubwa na bora kuwa na idadi kubwa ya mabao zaidi ya ile ya 2019/20,” alisema kocha huyo raia wa Ubelgiji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles