22.9 C
Dar es Salaam
Friday, May 27, 2022

Asasi yataka kasi uondoaji rangi zenye madini ya risasi

Godfrey Shauri –Dar es salaam

ASASI isiyo ya kiserikali ya Agenda, imeitaka Serikali kutoa elimu kwa wananchi ili kuharakisha ukomo wa matumizi ya rangi zenye madini ya risasi.

Agenda imeungana na wadau wengine duniani kukuza uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa kudhibiti rangi zenye madini ya risasi.

Ofisa Programu Mkuu wa Agenda, Silvan Mng’anya, alisema wanahimiza Serikali kuharakisha uondoaji wa rangi zenye madini ya risasi kwa kuweka hatua za kisheria.

Alisema Tanzania kupitia Shirika la Viwango (TBS) imeshaweka kiwango cha madini ya risasi katika rangi tangu mwaka 2017 ambacho ni sehemu 90 kwa milioni (90 ppm). Ofisa Programu Mwandamizi wa Agenda, Dorah Swai, alisema madini ya risasi yana madhara, hasa kwa watoto.

“Kwa watoto, madini ya risasi yanaweza kuathiri ukuaji wa ubongo na kusababisha upungufu wa uwezo wa mtoto kuelewa, mabadiliko ya tabia kama vile uwezo pungufu wa kuzingatia jambo, na ugumu wa kufikia malengo ya masomo.

“Pia madini ya risasi yanasababisha upungufu wa damu, shinikizo la juu la damu, matatizo ya figo, matatizo ya kinga ya mwili na matatizo katika njia ya uzazi,” alisema Dorah.

Alisema tafiti ambazo zilifanywa na asasi hiyo, asilimia 64 ya rangi za mafuta zilizokuwa zinauzwa nchini zilikuwa zimeshapunguza madini ya risasi.

“Kulingana na utafiti uliofany- wa na Agenda mwaka 2007, asilimia 64 ya rangi za mafuta zilizokuwa zinauzwa madukani zilikuwa zime- shapunguza madini ya risasi, hizi ni pamoja na zinazozalishwa nchini, hivyo inawezekana kuzalisha rangi ambazo hazina madini ya risasi,” alisema Dorah.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,429FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles