30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Chaula: Mpango wa anwani makazi kurahisisha biashara

Mwandishi Wetu -Dodoma

KATIBU Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Zainab Chaula, amesema ukamilishaji mpango wa anwani za makazi na postikodi unaotarajiwa kufikia halmashauri zote nchini ifikapo mwaka 2022, kutarahisisha shughuli za biashara mtandao na huduma za posta mlangoni.

Alisema hayo alipokuwa akizungumza wakati wa ziara ya kukagua uwekaji wa namba za nyumba katika kata tatu za Chamwino Ikulu, Ipagala na Hazina jijini Dodoma.

“Wizara ipo kwenye utekelezaji wa mkakati wa kuhakikisha kila nyumba inakuwa na anwani ya makazi inayojumuisha jina la barabara, mtaa na namba ya nyumba, ili wananchi waweze kufikiwa katika maeneo wanayoishi kwa urahisi na kukuza biashara mtandao na posta mlangoni kuelekea uchumi wa kidijitali,” alisema Dk. Chaula.

Mkurugenzi wa Idara ya Ma- wasiliano wa Wizara hiyo, Clarence Ichwekeleza, alisema mpango wa anwani za makazi na postikodi unatambulika kimataifa, ukamilishwaji wake utasaidia kuongeza fursa za kibiashara na kujiajiri, hasa kwa upande wa biashara mtandao ambapo wananchi wataweza kuagiza bidhaa na kuletewa hadi mlangoni.

Alisema utekelezaji wa zoezi hilo unahusisha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Tamisemi, halmashauri na wadau mbalimbali na kazi inayoendelea kwa sasa ni uwekaji wa namba za nyumba katika halmashauri za Jiji la Dodoma chini ya mkandarasi Suma JKT. Jumla ya nyumba 21,947 zi- tawekewa namba kati ya 30,152.

Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Justina Mashiba alisema ushirikishwaji wa Serikali na wananchi katika uwekaji vibao vya namba za nyumba ndio unaorahisisha kazi hiyo.

UCSAF imechangia Sh mil- ioni 60 kwa kata tatu za Chamwino Ikulu, Bahi na Hazina zilizopo jijini Dodoma.

Mpango wa uwekaji wa anwani za makazi na postikodi umetekele- zwa katika kata 116 nchini kati ya 3,956 kwenye halmashauri 18 kati ya 185.

“Mwitikio wa zoezi hili kwa wa- nanchi ni mzuri kwa sababu wenye manufaa kwa wananchi na Seri- kali katika ufikishaji wa huduma za dharura, biashara na huduma za posta.

“Faida nyingine za mpango huu kwa Serikali ni kurahisisha ukusan- yaji wa kodi, kuimarisha ulinzi na usalama kwa wananchi na kuhudumia wananchi wakati wa dharura za majanga ya moto na dharura ya wagonjwa,” alisema Mashiba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles