22.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

APANDISHWA KIZIMBANI KWA DAWA ZA KULEVYA

Na MANENO SELANYIKA-DAR ES SALAAM

MWANAMKE mmoja mkazi wa Tegeta kwa Ndevu jijini Dar es Salaam, Zena Hakika (32), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni kwa tuhuma za kupatikana na dawa za kulevya jana.

Wakili wa Serikali, Tumaini Mfikwa, alidai mbele ya Hakimu Boniface Lihamwike, kwamba tukio hilo lilitokea Januari 25, mwaka huu.

“Inadaiwa isivyo halali ulikutwa na dawa aina ya ‘Heroin Hydrochloride’ yenye uzito wa gramu 6.37 wakati ukitambua kwamba ni kinyume cha sheria ya Jamhuri ya Muungano,” alidai wakili.

Mtuhumiwa alikana kutenda kosa hilo ambapo upande wa Jamhuri uliomba tarehe nyingine ya kutajwa kwa kuwa upelelezi bado unaendelea.

Hakimu Lihamwike alisema shtaka hilo linadhaminika kisheria hivyo alimtaka mtuhuwa kuwa na wadhamini wawili walioajiriwa serikalini au katika taasisi yoyote inayojulikana kisheria.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 15, mwaka huu na mtuhumiwa aliachiwa huru baada ya kutimiza masharti ya dhamana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles