28 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

NG’OMBE AUA KIKONGWE

Na Ibrahim Yassin -Rungwe

WANANCHI wa Kijiji cha Mwela wilayani  Rungwe mkoani Mbeya, wameingia kwenye hali ya sintofahamu baada  ya mwanakijiji  mwenzao, Elizabeth Timba (80), kufariki dunia baada ya kupigwa teke na ng’ombe mali ya Mele Kibambo.

Tukio hilo la kushangaza na la kusikitisha    limetokea jana Kijiji cha  Mwela, ambapo kikongwe huyo alijikuta  akiingia  kwenye  wakati  mgumu, baada  ya kuvamiwa  na  ng’ombe huyo.

Mwenyekiti wa  Kitongoji  cha  Mwela,   Lwitiko  Mwambepo, alisema  baada  ya   kilio  na  vishindo  kusikika  maeneo  hayo, waliamua  kwenda eneo  la  tukio  wakiwa  wameongozana  na kundi  la  wananchi  na  kujikuta  wakibubujikwa  na  machozi,  huku  wengine  wakiangua  vilio baada  ya   kukuta  bibi  huyo akiendelea  kugaragazwa  chini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles