26.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 28, 2023

Contact us: [email protected]

UHIFADHI NYAYO ZA LAETOLI KUGHARIMU BILIONI 105/-

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

WIZARA ya Maliasili na Utalii inaendelea na jitihada za kutafuta vyanzo vingine vya fedha kugharamia utekelezaji wa mradi wa kuhifadhi nyayo za Laetoli kwa njia ya kisasa, Bunge limeelezwa.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Ramo Makani, amesema mradi huo unahitaji Sh bilioni  105  

  Amesema  hakuna hali ya kusuasua katika utekelezaji wa mradi huo  kwa vile  baadhi ya kazi  imekwisha kukamilika na nyingine ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Makani alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti maalum Hawa Mchafu (CCM).

Mchafu alihoji serikali ina mkakati gani wa kuajiri wataalamu hao ikizingatiwa Oktoba 25, mwaka jana, Televisheni ya  Mlimani  ilirusha kipindi cha urithi wetu   kilichozungumzia malikale za taifa.

Kipindi hicho pia kilieleza jinsi  agizo la Rais wa awamu ya nne, Dk. Jakaya Kikwete la ufunguzi wa nyayo hizo linavyosuasua.

Akijibu swali hilo, Makani alisema nyayo hizo ziligunduliwa na mtafiti Dk. Mary Leakey mwaka 1978 katika eneo la Laetoli ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro.

Naibu waziri alisema binadamu wa   miaka milioni 3.6 iliyopita waliweza kutembea wima kwa miguu miwili katika eneo hilo.

Alisema mwaka 2007 Rais Kikwete aliagiza wizara ifukue nyayo hizo na kuzihifadhi kwa njia ya kisasa itakayoruhusu matumizi ya elimu na utalii kwa watanzania na wageni na hifadhi hiyo igharamie kazi hiyo.

Alisema mradi unakadiriwa kugharimu takriban Sh bilioni 105 ambazo zingetumika kuwasomesha wataalamu, kuandaa michoro ya ujenzi wa makumbusho, kufukua na kuhifadhi nyayo, kusimamia ujenzi na kuweka mifumo ya uhifadhi.

Naibu Waziri alisema fedha hizo ni nyingi ikilinganishwa na mapato na majukumu ya mamlaka hiyo na hivyo wizara inaendelea na jitihada za kutafuta vyanzo vingine vya fedha   kugharamia utekelezaji wake.

Makani alizitaja kazi zilizokamilika kuwa ni   kuundwa  idara ya urithi wa utamaduni, kukamilika   michoro ya awali ya jengo la mapokezi, jengo la utafiti na jengo la elimu kwa umma.

Alisema    tathmini ya athari kwa mazingira imekwisha kuwasilishwa kwa mamlaka husika ikiwa ni pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco) kwa uchambuzi wa kina kwa lengo la kutoa idhini.

Vilevile mafunzo ya shahada ya uzamivu kwa watumishi wawili na kazi ambazo zinaendelea kutekelezwa ni kukamilisha taratibu za ajira kwa baadhi ya wataalamu wanaopatikana nchini. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles