27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Anayetuhumiwa kumkata kiganja mkewe akamatwa

NA GRACE MACHA – ARUSHA

MFANYAKAZI wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Ombeni Alfayo, anayetuhumiwa  kumshambulia mke wake, Veronica Kidemi (30) kwa kumkata kwa kitu chenye ncha kali na kutenganisha mkono na kiganja cha mkono wa kulia amekamatwa na kufikishwa Arusha.

Upelelezi wa tuhuma zake umekamilika, na jalada lake limepelekwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa taratibu za kisheria ili shauri hilo liweze kwenda mahakamani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Salum Hamduni aliwaaambia  waandishi wa habari ofisini kwake jana kuwa mtuhumiwa alikamatwa Dar es Salaam wiki iliyopita, na tayari amefikishwa kituo cha polisi wilayani Arumeru.

Alfayo anadaiwa kufanya tukio hilo Septemba 26, mwaka huu saa 5:45 asubuhi maeneo ya Siwandeti, Kata ya Kimyaki wilayani Arumeru.

Kamanda Hamduni alisema  uchunguzi wa awali unaonyesha wivu wa mapenzi ndiyo uliomsababisha Ombeni kumjeruhi mke wake, ambaye ni mwalimu wa Shule ya Sekondari Kiranyi.

“Mtuhumiwa alitoroka baada ya kufanya tukio hilo na tayari amekamatwa  Dar es Salaam, baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria,” alisema Kamanda Hamduni.

Alisema majeruhi Veronica anapatiwa matibabu Hospitali ya Selian jijini hapa.

Veronica akizungumza na waandishi wa habari akiwa hospitalini hapo, aliwaeleza kuwa mume wake, Alfayo amekuwa na kawaida ya kumtishia na kumfukuza mara kwa mara.

Alisema siku ya tukio, mume wake alimpigia simu akimtuhumu kuwa siku moja kabla alirudi nyumbani saa 12 akiwa amelewa jambo alilodai kuwa halikuwa na ukweli wowote.

“Ananituhumu kwa sababu ndiyo kawaida yake, hataki mtu atoke zaidi ya kwenda kazini na kurudi nyumbani, hataki hata uende dukani. Yuko Dar na mimi niko Arusha, hataki hata uende dukani, unaweza kufikiria ni mtu wa aina gani,” alisema Veronica.

“Aliniambia nichukue vitu vyangu, nisichukue watoto wake niwaache. Nikaona sasa simu zake zimezidi kunitisha nikaomba ruhusa kazini mchana ili niende polisi nikatoe taarifa, manake amezoea anakuja nyumbani bila taarifa hata usiku wa manane.

“Nimefika nyumbani nikamkuta, akanikimbilia, akawa anataka kunikata kata usoni nikawa nazuia na mikono ndiyo maana nikakatika huku kwenye mikono,” alisema Veronica.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles