20.8 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Amunike: Fei toto ni kiwango cha Barcelona, Ajib wakati wake waja

Lulu Ringo, Dar es Salaam

Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Emmanuel Amunike amesema mchezaji wa Klabu ya Yanga na timu ya Taifa, Feisal Salum (Fei Toto) anakiwango kikubwa cha kucheza mpira katika Bara la Ulaya.

Akizungumza na Mtanzania Digital leo Aprili 1, alipotembelea ofisi hizo, Amunike amesema juhudi anazoonyesha Feisal kama angekuwa Ulaya timu pekee ambayo ingemfaa ni Barcelona.

“Feisal anapambana sana ni mchezaji anayejituma na anajua nini anapaswa kufanya akiwa uwanjani, kama ingekuwa Ulaya basi angecheza Barcelona,” amesema Amunike.

Aidha kocha huyo amesema watu wengi wamekuwa wakilalamika mara zote anapoita kikosi cha timu ya taifa wakilalamika kwa nini anawaacha baadhi ya wachezaji hasa akiwemo mchezaji wa Yanga, Ibrahim Ajib pasipokujua kuwa timu ya Taifa inahitaji wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kupambana.

“Si kila mchezaji anayefanya vizuri kwenye klabu yake anaweza kufanya vizuri kwenye timu ya Taifa, Stars inahitaji wachezaji wanopambana kama mlivyoona kwenye mchezo wa mwisho na Uganda kila mchezaji alikua anapambana.

“Lakini hii haimaanishi kuwa Ajibu hafai kuitumikia timu ya Taifa, bado tunasafari ndefu wakati wake utafika na atakua mmoja kati ya wachezaji wa Timu ya Taifa,” amesema Amunike.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,058FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles