28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Azaki 65 zamuonya Msajili kuingilia migogoro ya vyama

Asha Bani, Dar es Salaam

Asasi 65 za Kiraia zimemtaka Msajili wa vyama vya Siasa Nchini aache kuvitisha na kuingilia migogoro ya ndani ya vyama vya siasa.

Aidha, badala yake wamemtaka aongozwe zaidi na hekima katika kusimamia misingi ya demokrasia na haki za wananchi kujiunga na vyama wanavyovitaka bila kuwekewa vikwazo visivyotambulika na sheria za nchi.

Wito huo umetolewa leo na Jukwaa la Wakurugenzi wa AZAKI katika ofisi ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, (LHRC), ambapo pia zimewataka viongozi waheshimu sheria za nchi na katiba kwa kuacha kuzuia mikutano ya siasa ya ndani na nje.

Akitoa tamko kwa niaba ya Azaki hizo, kuhusu hali ya demokrasia, haki ya kujumuika na kujiunga na vyama vya siasa, Onesmo Olengurumwa kutoka THRDC, amesema kumekuwa na matukio yanayoashiria ukiukwaji wa haki za kidemokrasia haki ya uhuru wa kukifanyika na kujiunga na vyama vya siasa.

“Kama Watanzania wenye jukumu kikatiba kulinda mshikamano, umoja,haki na amani ya nchi tumeona ni vyema kuzungumza na kuwashauri viongozi wetu wa kiasiasa kufuata sheria za nchi.

“Tumeshuhudia ukiukwaji wa haki hizo za kisheria na Katiba ya nchi ya mwaka 1977 na kwa kuwa asasi tumekuwa washauri na wakosoaji na wasaidizi wakubwa wa mambo mengi yakitaifa ni busara zaidi kulisemea hili ili kuhakikidha ukiukwaji wa haki hizi tajwa haziwezi kuwa sababu ya kupelekea kupoteza amani na umoja wa kitaifa,” amesema Olengurumwa.

Amesema katika kipindi cha miaka zaidi ya miwili hakuna demokrasia uhuru wa kujumuika na kujiunga na vyama zinazidi kuzorota kila kukicha.

Pia mwenendo wa muda mrefu wa Msajili wa vyama vya Siasa kuonekana kuchukua upande katika mgogoro wa ndani wa Chama cha Wananchi (CUF) na kusahau yeye ni mlezi wa vyama alipaswa kutokuwa sehemu ya mgogori ndani ya vyama.

Naye mwakilishi kutoka LHRC, Felister Mauya, amesema serikali inatakiwa kuhakikisha uhuru wa kujumuika ikiwa ni pamoja na uhuru wa kufanya maandamanao ya amani unaheshimiwa na kulindwa na vyombo vya usalama kama sheria zinavyoelekeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,455FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles