28.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Aliyechana Quran asimamishwa kazi

RAMADHAN HASSAN -DODOMA

WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo ameagiza kusimamishwa kazi kwa mtumishi wa Halmashauri ya Kilosa mkoani Morogoro Daniel Elimringi, kutokana na kuchana kitabu cha dini ya Kiislamu, Quran.

Kauli hiyo ya Jafo, inakuja baada ya kusambaa kwa picha katika mitandao mbalimbali ya kijamii zikimuonyesha mtumishi huyo katika Halmsahauri ya Kilosa kitengo cha biashara idara ya fedha akichana na kutupa kitabu cha Quran.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jana ofisini kwake, Jafo alisema ameamua kutoa maagizo hayo kwa Mkurugenzi wa halmashauli hiyo kumsimamisha kazi mtumishi huyo na hatua nyingine zichuliwe dhidi yake.

“Nayasema haya kutoka na kuwa mimi ni Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Tamisemi na huyu mtumishi yupo katika wizara yangu kwani Halmashauri ya Kilosa ni moja ya eneo langu hivyo natoa maagizo haya na yatekelezwe mara moja”alisema Jafo.

Aidha, alisema kuwa kitendo ambacho kimefanywa na mtumishi huyo hakipaswi kufumbiwa macho hivyo mkurugenzi wa Kilosa anatakiwa kuchukua hatua mara moja ya kumsimamisha kazi.

Pia, alisema mara baada ya kusimamishwa kazi mamlaka ya nidhamu ichukue nafasi yake katika kuchunguza suala hilo na baada ya kujiridhisha hatua kali zichukuliwe dhidi ya mtumishi huyo.

Vilevile, alimwagiza Mkuu wa mkoa wa Morogoro, pamoja na mkuu wa Wilaya ya Kilosa, kusimamia suala hilo na kuendelea kulinda amani na utulivu uliopo nchini.

“Jambo hili lililofanywa na mtumishi huyu halileti kabisa afya kwa taifa letu kwani watu wake wa dini zote wamekuwa wakiishi katika mazingira ya amani na kuheshimia kwa kila mtu”alisema Jafo.

Wakati Jafo akichukua hatua hiyo, taarifa zinadai kuwa tayari mtumishi huyo amefikishwa mahakamani na amenyimwa dhamana.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, kesi yake itatajwa tena Februari 20 mwaka huu.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles