25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mufti atoa tamko tukio la kuchanwa kwa Quran

Amina Omari, Korogwe

Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amewataka Waislamu nchini kuwa watulivu wakati vyombo vya sheria vikiendelea kuchukuwa hatua kwa tukio la kuchanwa kwa Quran.

Amesema kuwa kitendo cha kuchanwa kwa kwa kitabu kitukufu cha Quran kilichofanywa na Afisa Biashara wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, Daniel Malaki hakihusiani na mitazamo yoyote ya kidini.

Ameongeza kuwa kitendo hicho ni cha uzalilishaji wa maneno ya Mungu yanayopelekea kuwaudhi Waislamu na kusababisha kuleta mfarakano miongoni mwa jamii.

“Niwaombe Waislamu kuendelea kuwa na subira na uvumilivu huku wakisubiri kauli za viongozi wao wa Bakwata ambao wanafuatilia kwa ukaribu kesi iliyopo mahakama kwa sasa, “amesema Mufti Zubeir.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles