30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 30, 2023

Contact us: [email protected]

ADAMA BARROW APEWA MAKAO SENEGAL

DAKAR, SENEGAL


Adama BarrowRIPOTI kutoka nchini Senegal zinasema Rais mteule wa Gambia, Adama Barrow atabakia hapa hadi wakati wa kuapishwa kwake kipindi hiki ambacho Gambia iko katika mzozo.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya hapa, Rais wa nchi hii Macky Sall, amekubali kumpa makao Barrow jijini hapa hadi atakapoapishwa Januari 19 mwaka huu.

Uamuzi huo wa Sall, unasemekana umetokana na ombi la viongozi wa nchi za Afrika Magharibi.

Tayari Barrow yuko hapa baada ya kuvunjika kwa mazungumzo ya ujumbe wa nchi tatu ya kumshauri Jammeh kuachia madaraka Ijumaa iliyopita.

Rais wa sasa Yahya Jammeh amekataa kukubali kuwa alishindwa kwenye uchaguzi uliofanyika Desemba Mosi mwaka jana licha ya kuwa awali alikubali matokeo.

 

Juzi Rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keita, alimtaka Rais Jammeh kuondoka madarakani ili kuzuia umwagikaji wa damu.

Alikuwa akizungumza wakati wa mkutano wa Afrika na Ufaransa kwenye mji mkuu wa Mali, Bamako, ambao ulitawaliwa na mzozo uliopo Gambia.

Viongozi wa jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS wamemtaka Jammeh kuachia madaraka.

Tayari wakili wake ameitaka mahakama kuzuia kuapishwa kwa Adama Barrow

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles