24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

WABUNGE DEMOCRATIC KUGOMEA SHEREHE ZA KUAPISHWA KWA TRUMP

WASHINGTON, MAREKANI


Donald TrumpWABUNGE kadhaa wa Chama cha Democratic nchini hapa wamesema kuwa hawatahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule, Donald Trump, Ijumaa wiki hii.

Hii ni baada ya Trump kumshambulia Mbunge na mtetezi maarufu wa haki za binadamu, John Lewis aliyehoji uhalali wa ushindi wa Trump.

Lewis ni mmoja wa maspika ambaye bado wangali hai kati ya wanaharakati wa kutetea haki za binadamu, waliohudhuria mkutano wa kihistoria wa mwaka 1963 mjini Washington, ambao ulihutubiwa na mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu marehemu Martin Luther King.

Lewis, alisema hatohudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Trump kwa sababu hamtambui kama Rais aliyechaguliwa kwa haki kutawala Marekani.

Akijibu hilo,  Trump alisema kuwa hayo yote anayosema Lewis, ni maneno matupu yasio na matendo, huku akimshauri kushughulikia maslahi ya watu wa Wilaya yake ya Georgia.

Aidha mtoa maoni wa siasa za msimamo mkali, Bill Kristol, amesema kuwa Trump anampa Rais wa Urusi heshima kubwa mno.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles