29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

ACP Njera awataka waandishi  wa habari  wasiwe wanyonge

Na Malima Lubasha,  Musoma

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu Tarime/Rorya, Mara, ACP Mark Njera amewataka waandishi wa habari wasiwe wanyonge wakati wanatekeleza majukumu yao ya kihabari bali wazingatie weledi,maadili, sheria ili kuondoa migongano kati yao.

ACP Njera amesema hayo kwenye mdahalo baina  ya Jeshi la Polisi na waandishi wa habari juu ya  ulinzi na usalama uliofanyika katika  ukumbi wa Blue Sky mjini Tarime.

Amesema mdahalo huo umefungua ukurasa mpya na uwe chanzo cha kuondoa  tofauti kwa kuimarisha ushirikiano baina ya Jeshi la Polisi na waandishi wa habari katika kutekeleza majukumu yao kwa kuwa kazi zao zinaendana.

Ameeleza kuwa kila mmoja anapotekeleza majukumu yake ni lazima  kuzingatia kanuni na sheria  na kwamba Jeshi la Polisi limekuwa linatoa taarifa chache kwani kila jambo lina mipaka yake kuhusu usalama wao.

“Waandishi wa habari mnatakiwa kuandika habari za kweli zilizothibitishwa zinazoibua mambo yanayoleta tija kwa jamii kinyume chake zinaweza kuleta migongano baina ya taasisi na viongozi,” amesema Kamanda Njera.

Amesema amebaini baadhi ya changamoto zinazowakabili waandishi wa habari katika kutekeleza majukumu yao kwamba usalama  ni mdogo ambapo ametaka  uanze kwa mwandishi mwenyewe na wamiliki wa vyombo vya habari wawape mafunzo kuhusu usalama ikiwemo kuvaa mavazi maalum ya kumtambulisha anapokuwa kazini.

Aidha ACP Njera ameshukuru UTPC  kwa kuandaa mdahalo huo baina ya Jeshi la Polisi na waandishi wa habari  ambapo kwa matarajio ya kuwa na wazo moja kujadiliana ili kuondoa  changamoto zao katika kulinda jamii na mali zao.

Mwakilishi wa UTPC  katika mdahalo huo Edmund Kipingu, amesema  mdahalo huo umeandaliwa ili kuboresha mahusiano  baina ya  Jeshi la Polisi ambao huchukua hatua kwa wakosaji  na waandishi wa habari ambao kazi yao kuandika kuhabarisha umma hali inayoleta migangano.

Amesema  ili wawe marafiki  wanatakiwa  kushirikiana wanapotekeleza majukumu yao kwenye mabonanza, washirikishwe katika kutoa elimu kuhusu ukatili wa kijinsia kwani hiyo itakuwa ndiyo njia ya kuondoa changamoto baina yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles