32.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Chacha afariki kwenye harakati za kumnasa Kiboko

Na Malima Lubasha, Serengeti

Mkazi wa Kijiji cha Makundusi Kata ya Natta wilayani Serengeti mkoani Mara,Chacha Masaka(40)amefariki baada ya kusombwa na maji ya Mto Rubana akiwa katika harakati za kutaka kupata kitoweo cha mnyama kiboko huku wengine wakijeruhiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, ACP Salum Morcase amethibitisha kutokea tukio hilo lililotokea Desemba 3,2023 eneo la Mto Rubana majira ya saa 9.40 alasiri.

Kamanda ACP Morcase amesema katika tukio hilo, pia Mohoni Weisayi aling’atwa na kiboko huyo sehemu ya kifua na mgomgoni ambaye hadi sasa hawezi kuongea huku askari wanyamapori  kutoka Tawa, Elias Skeli akivunjwa mguu wa kushoto chini ya goti na kupelekea kulazwa hospitali ya Wilaya ya Serengeti.

Amesema kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa zimesababisha mito mingi kujaa maji hivyo kuwaleta kiboko hao kijijini hali iliyopelekea wananchi kuanza kuwashambulia kwa silaha za jadi ili kuweza kuapata nyama yake.

Kamanda ACP Morcase amesema kufuatia hali hiyo askari wanyamapori wa Tawa,Grumeti  na Polisi walikwenda eneo hilo kumdhibiti kiboko huyo ili asilete madhara kwa wananchi wakiwa katika harakati kwa kupiga risasi juu ndipo kiboko alimjeruhi Elias Skeli askari kwa kumvunja mguu na kufanikiwa kumpiga risasi kiboko.

Amesema baada ya hali hiyo kutokea kiboko alirudi kwenye maji mtoni akionekana kama mnyama huyo amekufa wananchi walifuatilia ili kupata kitoweo cha nyama ya kiboko huku askari wanyamapori wakidhibiti kwa kupiga risasi juu kuwazuia wananchi wasipate madhara katika harakati hizo ndipo Chacha aliposombwa na maji ambapo mwili wake umepatikana akiwa amepoteza uhai.

Kamanda Morcase anatoa wito na kuwataka wananchi wanapoona wanyama hao katika maeneo yao wachukue tahadhari ya kukaa  mbali wanaweza kujeruhi wakati wowote na kusisitiza kutoa taarifa kwa mamlaka husika ziweze kuchukua hatua ya kuwadhibiti wanyama hao.

Katika hatua nyingine Kamanda Morcase amethibitisha mkazi wa kijiji cha Kisangura Magembe Mairo (29)amenusurika kifo akiwa amelala na familia yake akiwamo mtoto wa umri wa miezi tisa baada ya mvua iliyoambatana na radi kupiga nyumba yake na kuteketeza vitu vyote vilivyokuwemo tukio ambalo limetokea Desemba 2, 2023 saa 4.00 usiku eneo la Kitongoji cha Kwigena.

Amesema Mairo akiwa amelala alisikia mungurumo wa radi na kuona miale ndani ya  nyumba hiyo ya nyasi  na inafuka moto, walipiga yowe kuomba msaada watu walijitokeza kuokoa lakini hawakufanikiwa vitu vilivyokuwemo  kwani moto ulikuwa mkubwa.

Alifafanua kuwa vitu vilivyoungua ni mabati tisa, godoro, mahindi, nguo na vyombo vya ndani, Pirau la ng’ombe vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 1.238.       

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles