Abdul Kiba: Nipo tayari kujiunga na Wasafi

Abdu KinaNA BEATRICE KAIZA

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Abdul Kiba, ameweka wazi kwamba yupo tayari kujiunga na lebo ya Wasafi inayoongozwa na msanii, Nasibu Abdul ‘Diamond’ anayedaiwa kuwa na ugomvi na kaka yake, Ali Kiba.

Abdul Kiba aliliambia MTANZANIA kwamba anachoangalia ni fedha kama Wasafi watamhitaji na watamlipa fedha za kutosha hatasita kujiunga nao na kutangaza lebo yao kwa kuwa ugomvi wa kaka yake na kiongozi wa kundi hilo haumhusu.

“Ninachojua Ali Kiba na Diamond hawana bifu lolote na kama wana bifu halinihusu mimi nafanya kazi na mtu au lebo yoyote itakayokidhi matakwa yangu,” alifafanua.

Msanii huyo anayetamba na wimbo wa ‘Bayoyo’ aliongeza kwamba licha ya kufungua milango kwa Wasafi, lakini yupo tayari kufanya kazi na mtu ama kampuni yoyote itakayokidhi mahitaji yake watakayokubaliana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here