29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga yaanza kuchanga karata

yngNA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM

WAWAKILISHI pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, timu ya Yanga jana walianza kuchanga karata zao kwa kuanza kufanya mazoezi kujiandaa na mechi za hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga inatarajia kucheza na Mo Bejaia ya Algeria Juni 17 nchini humo, mchezo ambao ni muhimu kwa Yanga kushinda kujiweka katika mazingira mazuri kusonga mbele.

Mazoezi hayo yalifanyika jioni Uwanja wa Taifa Dar es Salaam chini ya Kocha Hans Van De Pluijm na wasaidizi wake.

Wachezaji wapya waliohudhuria mazoezi hayo ni Hassan Kessy, Andrew Vincent na Juma Mahadhi, wengine wa zamani Oscar Joshua, Haruna Niyonzima, JumaAbdul, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Godfrey Mwashiuya, Pato Ngonyani, Amiss Tambwe, Ally Mustapha ‘Barthez’, Makapu, Matheo Anthony na Haji Mwinyi.

Katika mazoezi hayo, Pluijm aliwapanga katika vikosi viwili kikosi cha kwanza ni Cannavaro, Barthez, Oscar, Vincent, Haji, Mahadhi na Kessy, wakati kikosi B kilikuwa na Niyonzima, Tambwe, Matheo, Pato, Joseph Mhilo, Mwashiuya na Makapu.

Kikubwa walichokuwa wanafundishwa ni jinsi ya kufunga mabao ya mbali na kupasiana mpira, ambapo Kessy na Mahadhi walifunga bao moja huku Oscar akiweka kimiani mabao mawili.

Akizungumza wakati wa kumalizika mazoezi hayo, Pluijm alisema ndio wanaanza kujifua baada ya mapumziko mafupi waliyokuwa nayo.

“Tumeanza kujifua tutahakikisha tunafanya maandalizi safi ili tufanye vizuri katika michezo yetu, tumeanza na mazoezi ya kucheza mpira kwa kasi, kutoa pasi haraka na kufunga, tutazidi kufanya mazoezi ya nguvu,” alisema.

Wachezaji wa kigeni Thaban Kamusoko, Mbuyu Twite na Donald Ngoma, wanatarajia kuanza leo mazoezi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles